Latest News

BIO : KID INK


Kwa jina la kuzaliwa ni Brian Todd Collins ,amezaliwa 1,April,1986, ni mwanamuziki na pia produza wa Miondoko ya HIP HOP au RAP kutoka Los Angels huko Marekan, anayerekodi kazi zake chini ya label ya RCA records ambayo iliyochini ya Sony Entertainment.

Kid Ink aliachia Album yake ambayo aliyorecord peke yake , Up & away ambayo aliyoiachia 12,June ,2012 na sasa kuachia album yake ya Pili kwa jina la My own Lane ambayo inayohusisha singo tatu show me ft chris brown, iz u down, main chick ft tyga zilizokubalika zaidi katika Media .

Kid ink alianza muziki kipindi alivyokuwa yuko shule kwa kujifunza kurekodi mziki baada ya masomo... na alijuwa inspired na wasanii wakubwa kama Timbaland, Pharell williams na Swizz beats ...
Miaka inayofuta akaanza kazi kama Rapper wa muziki wa Hip Hop akiwa na Miaka 22.

kipindi cha mwaka 2009-2013...
Mwanahip Hop huyu hakuanza kuitwa Kid Ink bali alikuwa anaitwa Collins ...mara baada ya kukutuna na DJ III Will baada ya kupata upopulality  katika Mixtape yake ya World Tour ,ndio akabadilisha jina na kuwa KID INK...DJ III Will alimuanganisha kid katika label yake ya The Alumni na kuanza kazi zaidi iliyomfanya kutoa Mixtape 3 ambazo ni crash landing ,daydreamer na Wheels Up alizoshirikiana na wasanii wakubwa kama Roscoe Dash, Ty Dolla Sign, Meek Mill, Bow wow , Cory Gunz, Sean Kingston, Nipsey Hustle , 2 Chainz na wengine Kibao na kushilikiwa katika magazine ya XXL mnamo mwaka 2012 akiwa na wasanii kama Iggy Azalea, Macklemore, Future,Hopsin na Roscoe Dash.

Kid aliachia Album yake ya kwanza mwaka 2012,12- June iliyoitwa Up & away ambayo katika wiki yake ya kwanza  ilichukua No# 20 kwenye US BillBoard 200 .

Tarehe 4 ,january,2013 alitangaza kuwa amesign katika Label ya RCA records na kuachia Audio yake ya Bad Ass aliyomshilikisha Meek mill na Wale na  kushika chati katika list tofauti kama Billboard 100 kama #90 na Hot r&b/HipHop  kama #27...mnamo may ,28,2013 aliachia EP yake iliyoitwa Almost home ikishilikishwa wasanii kama French Montana, Meek Mill , Wale na wengineo ambayo iliyoshika nafasi ya No#27 katika Billboard 200...
Mnamo On September 17, 2013 aliachia singo ya album yake ya pili kwa jina la My Own Lane ,singo hiyo inayoitwa Show Me akimshilikiza Chris brown na kupewa Tuzo kutoka RIAA kwa singo hiyo, show me.

source : kid Ink @wikipedia 

CELEBRITY BLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

created & designed by obby hans. Theme images by Bim. Powered by Blogger.