Movie zinazotengenezwa Nollywood sasa hivi zimefika levo za kuuzwa kimataifa, wakiwa wanatengeneza zaidi ya movie 500 kwa mwezi za stori zinazohusu mapenzi, visa na visasi, comedy na uchawi, Nigeria pia ni nchi ambayo kwa wiki tu ina uwezo wa kutengeneza movie 50 na 30 zenye vigezo vya kimataifa.
Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa Tume ya Kimataifa ya Biashara inasema kwamba tasnia ya filamu Nigeria inachangia karibia dola Millioni 600 kwenye pato la taifa kwa mwaka ikiwa ni tasnia inayotengeneza zaidi ya movie 1,200 kwa mwaka na pia ni tasnia ya pili kwa ukubwa wakiongozwa na India.
Ripoti hio imeweka wazi kuwa Nollywood ni sekta kubwa ya pili inayoongoza kwa kutoa ajira Nigeria ikiongozwa na sekta ya kilimo.
No comments:
Post a Comment