Latest News

ukweli kuhusu BIG BROTHER AFRICA (BBA) 2015 huu Hapa...!


Kumekuwa na uvumi mkubwa juu ya shindano kubwa la TV Africa, Big Brother Africa (BBA) kutokufanyika mwaka huu na inadaiwa sababu ni ukosefu wa wadhamini wa shindano hilo.

Waandaaji wa shindano hilo, Africa Magic na Endemol wamesema shindano hilo la BBA 2015 linaweza lisifanyike mwaka huu na hivyo kuahirishwa mpaka mwakani.

Mshindi kutoka Tanzania wa Big Brother Africa Hotshot 2014; Idris Sultan.



Manager wa Multichoice Ghana, Anne Sackey amethibitisha uvumi wa taarifa hizo kwa kusema kuwa wao Multichoice Ghana walipokea taarifa kutoka MNET kuwa shindano la BBA mwaka huu halitofanyika kama ilivyozoeleka.

Anne Sackey
Anne Sackey amesema kuwa MNET hawajatoa sababu za kwanini shidano hilo halitofanyika mwaka huu lakini kwa upande wake anaamini kuahirishwa kwa shindano hilo ni kutokana na ugumu wa kupata wadhamini kwani kuendesha kipindi hicho hugharimu pesa nyingi sana.

CELEBRITY BLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

created & designed by obby hans. Theme images by Bim. Powered by Blogger.