Latest News

GOOD NEWS : nyimbo ya DIAMOND PLATNUMZ, NANA kushika No#1 kwenye RADIO U.K

Wasanii wengi wa Bongo Flava wamekuwa wakiiwakilisha Tanzania vizuri sana, wapo akina Joh Makini, Jux, Alikiba na wengine. Kwa kweli sitoacha kusema wasanii wetu wanajituma na kufanya kazi kwa bidii sana.

Good news nyingine tena inatoka Uingereza na inaandikwa Diamond Platnumz amabaye kwenye countdown ya DNA Top 5 kwenye radio ya BBC Radio 1Xtra kipindi kinachoendeshwa na DJ Edu wimbo wa Diamond ‘Nana’ aliomshirikisha Flavor kutoka Nigeria umesikika kwenye nafasi ya #1 wiki hii!


Licha ya hayo video ya ‘Nana’ ya Diamond Platnumz iliachiwa mwezi May tarehe 29 ambayo ni miezi 3 iliyopita lakini ukitembelea page ya Youtube ya msanii huyu muda huu utagundua kuwa kwa miezi hiyo 3 tu video hiyo imepata watazamaji Million 4+ na zaidi na kwa hilo well done Chibu!

Hii ndio Top 5 ya DNA Top 5 wiki hii kwenye BBC Radio 1Xtra..

Diamond feat. Flavour – Nana
Patoranking feat. Wande Coal – My Woman, My Everything.
Wizkid feat. Drake &Skepta – Ojuelegba (Rmx)
Khulichana feat. Patoranking – No Lie.
Davido feat. Meek Mill – Fans Mi.

CELEBRITY BLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

created & designed by obby hans. Theme images by Bim. Powered by Blogger.