Latest News

kuhusu KIFO CHA HUSSEIN MACHOZI ni UONGO (DEATH HOAX)

Usiku wa kuamkia leo zimesambaa habari za kwamba msanii wa muziki wa BONGO FLAVOR ,Hussein machozi amepata ajari na kufariki papohapo....


Hizi ni habari ambazo zimeanza kusambaa kwa watu kupitia Messenger (whatsapp) na pia Mitandao ya kijamii kama Facebook ,na Instagram..lakini SIO KWELI kama hussein machozi amefariki .

Kutoka kwa MILLARD AYO ,baada ya kupigiwa simu na watu wengi kutaka kujua kuhusu kifo cha Hussein,mnamo jioni ya jana jumatano ameeleza kuwa alipiga simu kwenye namba ya Hussein mwenyewe na akaanza kuongea hivii..

" Nilijiandaa hapa nimekwenda mazoezini kucheza mpira, niliacha simu yangu kwenye charge na niliporudi baada ya mazoezi nakuta missedcalls nyingi sana, msg na simu za mama yangu pamoja na dada, wakati najiandaa kuanza kupiga simu ghafla naanza kupata simu za watu mbalimbali kwamba nimepata ajali na kufariki, mimi nikawaambia sio kweli mimi ni mzima na nipo Dar es salaam " .
Kumbe baada ya taarifa za kifo kusambaa na kuwafikia Mama yake mzazi pamoja na dada yake ambao walipiga simu yake na haikupokelewa kwa muda mrefu, wakaamini kweli kilichotokea ni kifo…. mama akazimia hapohapo, dada akaanguka na kuzimia vilevile.


Sasa hivi Hussein inabidi alazimike kusafiri mpaka kwao Singida Manyoni ili kuwahakikishia ndugu zake kwamba yuko hai manake aliongea kwenye simu ya kaka yake na kumpa Dada simu baada ya kuzinduka lakini dada hajaamini, kasema anafichwa tu lakini ni kweli Hussein kafariki.

Mama anaendeleaje? ni yapi mengine ameyasema Hussein Machozi? bonyeza play hapa chini kumsikia mwenyewe…


CELEBRITY BLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

created & designed by obby hans. Theme images by Bim. Powered by Blogger.